Alhamisi 18 Septemba 2025 - 18:07
Mauaji ya halaiki huko Ghaza yanafichwa kupitia simulizi za kubuniwa

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Imani-Pour alisema: Yale yanayotokea Ghaza yanakutana na upotoshaji na kufichwa, wanafanya mauaji ya halaiki na jinai kisha wanadai amani, wanaua watoto wasio na hatia na wakati huo huo wanazungumzia uokoaji, wanatekeleza ugaidi, wanashambulia nchi nyingine na kisha wanazungumza juu ya urafiki na mataifa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Imani-Pour, rais wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu, katika mkutano wa nane wa viongozi wa dini za dunia na jadi nchini Kazakhstan, alisisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tangia mwanzo imekuwa msaidizi na mshirika wa mkutano huu, na imekuwa ikiuunga mkono kwa shauku juhudi za kijasiri za kuweka mfumo katika shughuli za pamoja baina ya dini kwa lengo la kueneza amani yenye uadilifu, na itaendelea kufanya hivyo.

Akaongeza kuwa: Mada ya kipindi hiki cha mazungumzo ni mshikamano wa dini kwa ajili ya mustakabali na uchambuzi wa changamoto na fursa zilizopo mbele yetu, bila shaka tuko katika moja ya nyakati zilizojaa changamoto zaidi katika maisha ya mwanadamu; kushughulikia changamoto zote si jambo linalowezekana, lakini mimi nilijikita katika mada ya utumwa wa kidijitali kama moja ya changamoto kuu na njia za kuondokana nazo kwa mfumo wa mshikamano wa dini.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Imani-Pour, akibainisha utegemezi mkubwa wa maisha ya kila siku kwa intaneti, mitandao ya kijamii na huduma za kidijitali, alisema: Utegemezi huu unawasukuma watumiaji kuelekea vifurushi vya huduma na mifumo ya kidijitali inayodhibiti maamuzi makuu ya dunia ya sasa, aina hii ya utegemezi inaweza kuleta vizuizi katika uchaguzi na uhuru wa kufanya mambo, jambo linalofanana na utumwa wa kiuchumi au kitamaduni  algoriti za kisasa zinatabiri na kuelekeza mienendo ya watumiaji, mara nyingine hata bila mtu kutambua udhibiti huo.

Aidha alisema: Mada ya haki za binadamu katika anga ya kidijitali ni muhimu sana, mazingira ya kidijitali yanaweza kuunda sura mpya ya ukoloni na unyonyaji wa kibinadamu, wafanyakazi wengi wa kidijitali, kama wale wanaotoa huduma mtandaoni, kutengeneza maudhui au kusimamia data, hufanya kazi katika mazingira yasiyo na usalama wa ajira na haki stahiki, hali hii ni mfano wa utumwa wa kisasa wa kidijitali, kwani kimsingi ni unyonyaji wa kazi ya mwanadamu ndani ya mfumo wa teknolojia.

Rais wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu alisisitiza: Vyombo vya habari havipaswi kubadilisha ukweli na kuonesha mambo tofauti na yalivyo, wakibadilisha nafasi ya shetani na malaika, tunaishi katika zama ambazo tawala haziwajibiki mbele ya madai ya wananchi na mifumo ya kimataifa na taasisi za haki za binadamu hazina ufanisi, ni matarajio gani yanaweza kuwepo kwamba wenye “data kubwa” watatumia rasilimali zao kwa ajili ya kufikisha ukweli?

Raisi huyo pia alionya kuhusu utawala wa data na wenye taarifa kubwa na matumizi yake katika vita vipya vya mchanganyiko: Sasa hivi kuna juhudi kubwa za kupotosha na kuficha ukweli mitandaoni, baadhi ya machapisho na maoni ya watumiaji hufutwa kwa kisingizio cha kuchochea vurugu au chuki, ilhali yale ya vyombo vya habari vinavyotawala huruhusiwa, mfano ni yale yanayoendelea Ghaza, ambako yanakumbwa na upotoshaji na kufichwa, wanatekeleza mauaji ya halaiki na jinai, lakini wanadai amani, wanaua watoto wasio na hatia na wanazungumzia uokoaji, wanatekeleza ugaidi, wanashambulia nchi nyingine na wanazungumza juu ya urafiki na mataifa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha